PANGANI JOGGING CLUB YAZINDULIWA KWA KISHINDO


Mbunge wa PANGANI na naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mh jumaa awesso akikata utepe ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Wa tatu toka kushoto) akiwa na Kamati na wajumbe wa awali wa PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja
Kamati na wajumbe wa awali wa PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso akiwa na wana-PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Mbele) akiwa katika mazoezi na Wana-PANGANI JOGGING CLUB mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Maulidi Kitenge wa Efm sambamba na afisa tawala wa Pangani ndugu Gibson George wakati wa uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB walipokuwa wakikimbia katika mji huo wa kihistoria.
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso akiwa katika mazoezi ya viungo na Wana-PANGANI JOGGING CLUB.

Zaidi ya watu mia tano wamejitokeza katika uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB uliyofanyika asubuhi ya Jumamosi ya tarehe 24/11/2018 katika uwanja wa Bomani Pangani mjini. 

Uzinduzi huo umepambwa na mazoezi ya pamoja, yaliyoendeshwa na club ya mazoezi kutokea jijini Tanga, Power and Sports ambayo yalinogesha na kuongeza hamasa kwa umati mkubwa ulihudhuria uzinduzi huo wa kihistoria. 

Mbali na Power and Sport, club nyingine zilizoshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na TK Jogging club kutokea jijini Tanga, na EFM jogging club kutokea jijini Dar es salaam ambayo baadae ilicheza mchezo wa soka wa kirafiki dhidi ya wakazi wa Pangani.

Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB alikuwa ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Na Mbunge wa Pangani Mh. Jumaa Awesso ambaye mbali na kushiriki mazoezi na wananchi wake, pia amekubali kuwa mlezi wa club hiyo,Pia katika kutambua umuhimu wa michezo na Mazoezi Mh Aweso alitoa zawadi ya mipira kwa klabu za soka wilayani Pangani

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali, waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara halmashauri ya Pangani pamoja na wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi

PANGANI JOGGING CLUB imezinduliwa ikiwa na lengo la kuhamasisha mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya, kwa mustakabali wa maendeleo ya Pangani, sambamba na kuhamasisha ushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kukuza mahusiano ya watu na kubadilishana mawazo, pamoja na kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo za serikali.

Afisa Tarafa wa Pangani mjini na Mwenyekiti wa club hiyo Bi. Zuhura Rashid, sambamba na katibu wake Bwana Midraj Msusa, wamemesema kuwa, club hiyo itakuwa endelevu, na itasaidia kwa kiasi kikubwa wanapangani katika mustakabali wa kupambana na afya zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527