POLISI TANGA WADAI KUUA MAJAMBAZI WATATU

Polisi mkoani Tanga limewaua watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi Jumapili Novemba 25, 2018 katika majibizano ya kurushiana risasi mtaa wa Ngwaru Kanisani kata ya Kwemkabala Muheza mjini wakitumia katika jaribio la kutaka kupora fedha.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe amesema majambazi hao walikuwa na gari aina ya Toyota X- Trail rangi nyeusi ambapo polisi walilipiga risasi kwenye matairi na kushindwa kutembea.

Amesema majambazi hao walikuwa katika jaribio la kuvamia nyumba ya mfanyabiashara maarufu mjini Muheza, Jackon Mhufu kwa lengo la kutaka kupora fedha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo majambazi hao walianza kurushiana risasi na askari polisi baada ya kuzidiwa walianza kukimbia huku na kule ndipo wananchi wakatoa ushirikiano na kufanikiwa kuuawa kwao.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali teule ya mtakatifu Augustine Muheza kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwemo kuwatambua majina.

Hii ni mara ya pili kwa majambazi hao kumvamia mfanyabiashara huyo kwa jaribio la kutaka kupora fedha lakini Polisi wilayani Muheza walifanikiwa kuwadhibiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527