BINTI AOLEWA KWA MAHARI YA MILIONI 20, NG'OMBE 520, MAGARI MATATU


Nyalong Ngong Deng, akiwa na mume wake Kok Alat.

Hatimaye familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na wanaume wengi walioahidi kutoa mahari kubwa zisizo za kawaida, ameolewa kwa mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8.

Mrembo huyo, Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka, ambapo kila mmoja alikuwa tayari kutoa mahari kubwa ikiwa ni pamoja na shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Tanzania.

Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9,2018 binti huyo wa kabila la Dinka aliibua mshangao kwa watu waliokuwa katika sherehe hiyo.

Kulingana na utamaduni wa Dinka na Nuer, bei ya mahari kwa kawaida ni ng'ombe 20 hadi 40 hivyo binti huyo ameandika historia ya pekee katika kabila lake kwa kuolewa kwa mahari ya ng'ombe 520 na vitu vingine vya thamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527