MSEMAJI WA SERIKALI AZUNGUMZIA MKANGANYIKO SAKATA LA USHOGA


Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas

Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amesema masuala na misimamo ya kitaifa nchini inatolewa na mtu ambaye ana mamlaka ya kitaifa na si mtu mwingine ambaye mamlaka yake yapo kwenye ngazi ya idara, au taasisi nyingine za serikali.

Akijibu swali na mwandishi wa habari katika mkutano ambao alikzungumzia juu ya mafanikio ya serkali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitatu ambaye alihoji juu ya mkanganyiko juu utekelezaji wa kampeni aliyoianzisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kupambana na wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Dkt Abbaasi amesema “Serikali ina mfumo ambao uko wazi, mfumo wa serikali una msemaji katika kila ngazi inapokuwa masuala ya kitaifa ni kati ya msemaji mkuu ni au viuongozi wakuu wa kitaifa pale ambapo kiongozi akitoa tamko kuhusu jambo la kitaifa si tamko la serikali, akitokea katibu kata anazungumzia jambo la kitaifa hilo sio lake.”,

Aidha Dkt Abbas amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameahidi kuendeleza kutekeleza ahadi zake ambazo amezitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

“Nchi yetu imesogea sana kiuchumi na unakuwa kwa asilimia 7.1 na tumeongeza ukusanyaji wa mapato kupitia watanzania wanavyojitolea kuhusu kulipia kodi, na pia tumejitahidi kuinua mashirika ya serikali kwa kufanya mageuzi kwenye utendaji.” ameongeza.
Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527