MBARONI KWA KUMKATA SIKIO MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI BULIGE - KAHAMA

Zaituni Said akiwa amekatwa sikio

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zaituni Said (22) mkazi wa kijiji cha Bulige kata ya Bulige katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga amenusurika kufa baada ya kukatwa sikio kwa kisu na mmewe aitwaye Lucas Gerendo(33).


Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jana Novemba 9,2018 majira ya saa tatu usiku wameiambia Malunde1 blog kuwa mwanamme huyo alimvizia mkewe akienda kusali kanisani. 

“Dada huyu ameachana na mmewe kama mwezi mmoja hivi akawa kwao,akiwa kwao akawa kwenye maombi,walikuwa wamefunga,kabla ya kwenda kwenye maombi huyo bwanaake akawa amempigia simu,akamwambia kata simu yako,simu yangu imeishiwa chaji,akaenda kanisani….basi yule bwana akaamua kumvizia kwenye njia ya kanisani akiwa ameshikilia fimbo na kisu akaanza kumchapa na kumkata sikio la mkono wa kulia"....

“Alivyomkata vile akampeleka yeye mwenyewe nyumbani kwao na mwanamke,alivyofika akamwita mama mkwe kisha kaanza kumwelezea mama kuwa amemkuta mwanae kakumbatiwa na wanaume wawili,akaanza tena kumchapa mbele ya mama mkwe huku akimvuta kanga mama mkwe huyo aliyekuwa amevaa kanga moja tu,pakatokea msala mwingine”, 

“Sasa huyo mama mkwe baada ya kuvutwa kanga yake,akashtuka kumuona mwanae anatokwa damu nyingi,akamuuliza vipi,binti akajibu amenitoa na sikio,jamaa akakimbia”, wameeleza.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Zaituni akiwa nyumbani kwake aling'atwa sikio lake la kushoto sehemu ya juu na kunyofolewa kipande na mume wake aitwaye Lucas Gerendo mkazi wa Bulige. 

Kamanda Mutalemwa amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo mume alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine. 

Amesema majeruhi amepatiwa   matibabu katika kituo cha Afya Bulige na Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa hatua zaidi za kisheria. 


Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527