Wednesday, November 14, 2018

MCHEZO MPYA WA SUPA TANO WAZINDULIWA TANZANIA

  Malunde       Wednesday, November 14, 2018
Meneja wa Fedha wa kampuni ya The Network. Jacob Millinga akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu  namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry  maarufu kama Monalisa kwa Wanahabari leo jijini Dar.
Balozi wa Supa 5 Adam Mchovu akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari namna ya kucheza mchezo huo wa namba ujulikanao kama Supa 5 kupitia simu ya mkononi,ambapo mshindi 
anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
Uzinduzi wa Mchezo wa namba ujulikanao kwa jina la Supa 5 ukiwa tayari  kuzinduliwa rasmi na wananchi kuanda kuucheza mchezo huo kwa njia ya  simu zao za Kiganjani.

**


• Kwa shilingi 1,000 tu mchezaji anaweza kushinda hadi 10,000,000/- kila baada ya dakika 10Kampuni ya The Network inayosimamia michezo ya namba nchini Tanzania leo imezindua mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni 10,000,000/- kila baada ya dakika 10.

Huuunakuwa ni mchezo pekee kwa sasa nchini Tanzania ambapo mshindi anawezakupata kiasi kikubwa ndani ya dakika kumi tu. Mchezo wa Supa Tano pia unakuwa ni mchezo pekee wenye kutoa fursa nyingi zaidi za ushindi hapa  nchini.

Meneja wa Fedha wa The Network,Bwana Jacob Millinga, amesema ‘SupaTano ni mchezo mpya wa namba ambao wachezaji wanaweza kucheza viwango mbalimbali kati ya shilingi 1000 mpaka 20,000. 

Mchezo unatoa nafasi ya kushinda hadi mara 10,000 ya dau uliloweka, ambacho ni kiasi kikubwa 
kuliko mchezo wowote Tanzania’ anasema Kupitia Supa Tano mchezaji anapata nafasi nyingi zaidi za ushindi, kwani kila namba anayolinganishaanalipwa kuanzia namba 2, 3, 4 au namba 5 kwenye droo za kila dakika 10, na wakati huo huo kila shilingi 1000 yake inampa nafasi ya kuingia kwenye SupaMzuka Jackpot siku za Jumapili na Jumatano.

‘Mchezaji  anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo  zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya 
simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa.

Mchezo wa Supa 5 unaendeshwa kwa uwazi na usimamizi wa serikali kupitia Bodi  ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Matokeo yote ya washindi na zawadi walizoshinda yatawekwa kwenye tovuti ya: www.supatano.co.tz.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwakilishi wa Bodi ya michezo ya Kubahatisha  Tanzania (GBT), amesema mchezo wa Supa 5 unaongeza fursa nyingine za ushindi kwa watanzania lakini ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa ustaraabu bila kutumia pesa ya matumizi muhimu kwenye mchezo huu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post