HIZI APPS HIZI ZINA UWEZO WA KUIBA TAARIFA ZAKO ZA BENKI,EMAILS NA PASSWORDS ZAKO

Kama ukiangalia katika simu yako  nina uhakika Application nyingi ulizopakua ni za bure.Wote tunapenda App za bure. 

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako. 

Je unasomaga vigezo na masharti kabla ya kuipakua hiyo Application na kuiweka kwenye simu yako? Ninauhakika jibu na HAPANA.

Wengi huwa tunabonyeza tuu ‘Agree’ katika vigezo na masharti, kitu ambacho ni kosa kubwa.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue  ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Tuende moja kwa moja kwenye mada ya leo.Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUSaina ya TROJAN

Kwa mujibu wa utaifiti huo, virusi hao ambao hutumia majina tofauti tofauti wanauwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa Hackers(Wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zinauwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing)  ambapo ukijichanganya tu basi taarifa zako za siri kama bank details,email, password zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa Hackers.

==>Baadhi ya App hizo ni:    
Daily Horoscope – Astrological Forecast
Master Cleaner – CPU Booster     
Speed Cleaner – CPU Cooler
Master Clean – Power Booster    
Horoscope 2018
Super Fast Cleaner 

Ni imani yangu makala hii imekufungua macho na utakuwa makini zaidi ili kujikinga na wadukuzi wa mitandaoni.

<<INGIA HAPA>> Kuzijua App zote 29 ambazo zina virusi ndani yake. Kama ulizipakua basi zifute kabisa kwenye simu yako.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527