SERIKALI YAUKATAA MPANGO WA UFUNGAJI MGODI WA BUZWAGISerikali imeitaka kampuni ya Acacia kuandaa na kuwasilisha haraka mpango mpya wa urejeshaji mazingira katika hali yake ya kawaida baada ya kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ifikapo mwaka 2020.


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyasema hayo jana alipofanya ziara katika mgodi huo kukagua shughuli zinazoendelea mgodi hapo.


Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliukataa mpango uliokuwa umeandaliwa na kampuni hiyo ukikadiriwa kutumia dola milioni 18 kwa kuwa haukujumuisha kufukiwa baadhi ya mashimo mgodini hapo (tazama picha), bali yabaki wazi hadi yatakapojaa maji katika kipindi cha miaka 100 ijayo. 

Na George Binagi-GB Pazzo
Naibu Waziri Doto Biteko (katikati), akifafanua jambo wakati akikagua shughuli mbalimbali katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Doto Biteko akielekea kukagua sehemu ambapo mchanga wenye madini (makinikia) umehifadhiwa ndani ya mgodi wa Buzwagi.
Tazama Video hapa chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527