WATU 8 WANAODAIWA KUWA WAHAMIAJI HARAMU WAFARIK BAHARINI TANGA

Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga imekiri kutokea kwa vifo vya watu 8 ambao wanatajwa kuwa ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani walikuwa wakisafiri kupitia bahari ya hindi kuingia nchini.

Akizungumza Mkoani humo ofisa uhamiaji mkoani Tanga, Ally Dady amesema watu hao wanatajwa kuwa ni raia wa Ethiopia walitokea nchini Kenya, ambapo miili yao iliokotwa na wavuvi waliokuwa wakiendelea na shughuli zao za uvuvi.

“Waethiopia 8 walipata ajali baharini wakisafiri kutoka Kenya na kuja Tanzania, wavuvi na wanakijiji walisaidia kupatikana miili 8 ya wahamiaji hao haramu”, amesema Ofisa huyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward, Bukombe amesema jeshi hilo litawafikisha mahakamani baadhi ya manusura wa ajali hiyo kwa kuingia nchini bila kibali.

“Juhudi zilifanyika za kufatilia miili ya watu 8 ambao jumla yao walikuwa 13, na baadhi waliobakia watafikishwa mahakani kwa makosa mbalimbali”, amesema Kamanda Edward Bukombe

Mpaka sasa miili ya wahamiaji hao imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kukabidhiwa ofisi ya ubalozi ili kufanya utaratibu wa mazishi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post