BASATA WAFUNGUKA SAKATA LA VIDEO ZA NGONO WASANII BONGO..WEMA,AMBER RUTTY KUKIONA


Baraza la sanaa Taifa (BASATA) limefunguka juu ya tukio la kusambaa ka video ya ngono ya msanii na video queen, Amber Ruty, na kumchukulia hatua kali za kinidhamu.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, amesema kwamba msanii huyo amevuka kiwango cha uhayawani, na kutaka mtu au taasisi yoyote kutofanya kazi na msanii huo.

“Kuna mmoja ameenda mbali kabisa amevuka hata kiwango cha uhayawani, na imeleta taharuki sana katika jamii, huyu Amber Ruty huyu, halafu hata hashtuki, sitarajii kwamba huyu atakuja nimsajili kama msanii, sitarajii, huyu anachafua kwa makusudi kabisa sanaa, na nitamke wazi kuwa mtu yeyote au taasisi yoyote itakayofanya naye kazi ya sanaa, huyu Amber Ruty, Baraza halitasita kuchukua hatua”, amesema Mngereza.

Wakati huo huo Katibu huyo wa BASATA amezungumzia juu ya msamaha aliouomba jana muigizaji Wema Sepetu, na kusema kuwa ni unafiki mkubwa kwani sio mara ya kwanza wala ya pili kwake.

“Hii ni kama unafiki fulani, kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyu, wala sio mara ya pili, na niseme tu kwamba kwa upande wa Baraza lina mchango wake kufikia hapo alipofikia, ile ni unafiki, haitoshi, mmtu mara ya kwanza ya pili unasema hii ni tabia zake, na kwa vile kuna sheria zingine zilizovunjwa, lazima wahusika wachukue hatua zake, hii haitoshi, lazima awe mfano”, ameongeza.

Hapo jana msanii Wema Sepetu aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuomba msamaha kwa tukio lake la udhalilishaji na kuaibisha la kusambaa kwa video yake chafu ya ngono.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post