MAKONDA AMTAKA AMBER RUTTY KUFIKA POLISI...SAKATA LA VIDEO YA NGONO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia), na Amber Rutty.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza msanii wa muziki wa bongo fleva mwanadada Amber Rutty kufika kituo chochote cha Polisi jijini humo kabla ya saa 12 Jioni.


Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha picha ya mwanadada huyo na kuandika, "wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya saa 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na RC Makonda watakupatia ujumbe wako".

Video ya mwanadada huyo yenye maudhui ya kingono, imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua taharuki kubwa kwa jamii na vyombo vinavyohusika na kusimamia wasanii ikiwemo BASATA.

Tayari msanii, Amber Rutty amejitokeza na kuomba radhi kutokana na kusambaa kwa video hiyo, huku akishindwa kufafanua mazingira ya kurekodiwa na hata kusambaa kwake. Baraza la sanaa Taifa (BASATA) imefunguka juu ya tukio la kusambaa kwa video hiyo na kuahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post