Familia ya Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji imetangaza zawadi nono ya TSH. BILIONI MOJA (1,000,000,000) kwa yeyote atakaetoa taarifa muhimu zitakazofanikisha kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo alietekwa.
Dau hilo limetangazwa leo October 15, 2018 na msemaji wa familiahiyo , Azim Dewji, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za MeTL zilizopo jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es Salaam.
Familia imesema Mwenye taarifa anaweza kuwasiliana na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755030014, 0717208478 na 0784783228 na findmo@metl.net
"Familia inaahidi kwamba Mtoa taarifa pamoja na Taarifa vitabaki kuwa ni siri kubwa baina ya Mtoa taarifa na familia" -Amesema
Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Alhamisi Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Collosseum jijini Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.