TAMUFO YAZUNGUMZA NA MAOFISA WA POLISI KURASINI KUHUSU SHERIA YA KULINDA KAZI WA WANAMUZIKI NCHINI

 Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga (katikati), akizungumza na Maofisa wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu haki za kazi za wanamuziki hapa nchini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel na kulia ni mtoa mada, Mkaguzi wa Polisi Dkt.Ezekiel Kyogo.

 Maofisa wa Polisi wa chuo hicho wakifuatilia mada hiyo.
 Mada ikiendelea.
 Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel , akizungumza na maofisa hao.
 Maofisa hao wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga (kushoto), na Katibu wake Stellah Joel wakiondoka eneo la mkutano baada ya kutoa mada kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu haki za kazi za wanamuziki hapa nchini. 
Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga (kulia), na Katibu wake Stellah Joel (katikati), pamoja na Mkaguzi wa Polisi, Dkt, Eekiel Kyogo, wakiwa wamesimama mbele ya Jengo la Chuo cha  Maofisa wa Jeshi la Polisi  Kurasini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kutoa mada kuhusu haki za kazi za wanamuziki hapa nchini. 


Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), umetoa mada kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo  Chuo cha Polisi cha Kurasini jijini Dar es Salaam kuhusu haki za kazi za wanamuziki hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga alisema lengo la mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa hao ni kuwajengea  uelewa wa ulinzi wa kazi za muziki ikiwepo  kudhibiti na kuwakamata maharamia wa kazi za wanamuziki hapa nchini.

Katibu Mkuu wa TAMUFO Stellah alisema umoja huo ulishatoa mapendekezo kupitia waraka maalumu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harisson Mwakyembe ili mtu yeyote atakayebainika akihujumu kazi za wasanii ashitakiwe kwa makosa ya jinai.

Alisema TAMUFO pia inaandaa mapendekezo ya kupeleka serikalini ya kuweka dawati la jinsia katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini ambayo yatakuwa yakishughulikia wizi wa kazi za wanamuziki.

Mkukaguzi wa Polisi Dkt. Ezekiel Kyogo akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyowahusisha maofisa wa polisi zaidi 500 kutoka mikoa yote ya Tanzania alisema ni muhimu kwa maofisa hao kujua sheria hizo kwa kuwa wao ndio wanaozisimamia.

"Changamoto kubwa tuliyonayo ni maofisa wetu wa polisi kutojua sheria zinazosimamia kazi za wasanii wetu ndio maana tumeona tuwapige msasa ili waijue na kuweza kuongeza nguvu ya kuwakamata maharamia wa kazi hizo za wanamuziki" alisema Kyogo.


Alisema sheria ya mtandao ya mwaka 2015 sheria namba 14 mtu yeyote atakaye bainika akidurufu nyimbo na kumpa mtu mwingine bila ya ruhusa ya mmiliki wa wimbo husika adhabu yake ni kifungo kisicho zidi miaka mitatu au kulipa faini shilingi milioni tano.

Aliongeza kuwa kwa mtu atakayebainika akidurufu nyimbo za wasanii kwa lengo ya kuziuza kifungo chake ni miaka mitatu au kulipa faini shilingini milioni 20 hivyo alitoa  rai kwa wananchi kuacha kuchezea kazi za wasanii kwani sheria hizo zipo na zinafanya kazi.

Alisema kazi za wasanii zikilindwa zitawanufaisha kwa kuziuza na zitatoa ajira hivyo ni muhimu jamii ijengewe uelewa ili waache kuiba kazi hizo ambazo zikilindwa vizuri zitaweza kutangaza utamaduni wetu na serikali itapata mapato kutokana na kodi watakazolipa wahusika baada ya kuziuza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527