RC Makonda aibuka na 'List' nyingine Ya MashogaMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefunguka kuwa mpaka sasa ametumiwa ujumbe mfupi wa maandishi wenye majina ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja 'mashoga' zaidi ya 100 katika mkoa wake.


Taarifa iliyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam, imesema kuwa mpaka sasa amepokea meseji 5763 zenye majina 100 ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

“Nimepokea meseji zaidi ya 5763 na majina ya mashoga zaidi ya 100, hii inaonyesha wana Dar es salaam hawataki mashoga, naendelea kupokea majina ya mashoga", amesema Makonda.

Jana katika mkutano wake na wanahabari Makonda alisema kuwa wazazi wengi nchini wamekwazika na vitendo vinavyofanywa na vijana mitandaoni ikiwemo kutuma picha zisizo na maadili na kwamba ataendesha zoezi la kuwakamata watu hao katika mkoa wake. "Jambo hili linaendelea kupoteza utu na staa na kwakua mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika na matumizi mabaya ya mitandao sasa nimeamua kuendesha zoezi la kuwakamata Watu wote wanaofanya vitendo hivi vya aibu, zoezi hili litaanza Jumatatu makundi ya mashoga, wanaotuma na kufanya biashara ya ngono mitandaoni na wale wanaojipatia pesa kwa njia ya utapeli", amesema Makonda.SOURCE:EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post