MOTO WAIBUKA KATIKA JENGO LA BENJAMIN MKAPA

Moto umezuka leo katika jengo la Benjamin Mkapa, Millennium Tower – Dar ambapo unasadikiwa umeanzia kwenye ghorofa ya tatu. 

Mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zimamoto na uokoaji, Elinimo Shang'a amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ilioanzia stoo.

Amesema kutokana na uwazi katika chumba hicho moshi ulisambaa na kusababisha taharuki.

Kuhusu madhara amesema hakuna madhara kwa mtu yeyote lakini uchunguzi unaendelea kujua hasara iliyopatikana.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.