MAKONDA AFUNGUKA TENA SAKATA LA VIDEO ZA NGONO ZA AMBER RUTTY

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amefunguka tena kuhusiana na video chafu za mrembo Amber Rutty na mpenzi wake lakini pia kuhusiana na ongezeko la mashoga katika jiji la Dar es Salaam.


Akiongea na waandishi wa habari jana October 29, 2018, RC Makonda alisema kuwa Amber Rutty na mpenzi wake bado wapo lupango wakati wanasubiriwa kupandishwa kizimbani na kuweka wazi kuwa adhabu yao ni kifungo cha maisha jela au miaka 30 kama itatbitika wanafanya kinyume na maumbile."Tayari yule binti anayeitwa Amber Rutty pamoja na bwana yake wapo chini ya polisi tangu kipindi kile nilivyotoa maelekezo na niseme kuwa kosa lile liko wazi na sheria inasema ni aidha kifungo cha maisha au miaka 30, hiyo yote ni kuonyesha ni jinsi gani serikali isivyopendezwa na mienendo inayomomonyoa maadili ya taifa letu”. Alisema Makonda


Lakini pia RC Makonda alitangaza vita na mashoga wote ambao wanajihusisha na shughuli za kufanya mapenzi kinyume na maumbile;


"Naomba nitoe fursa hii kwa wakazi wa Dar es Salaam, namba yangu ya simu inafahamika .Nimepata taarifa kwamba kuna mashoga wengi sana kwenye mkoa wetu na mashoga hawa ndio kazi yao wanajinadi kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo nawaambia wananchi kama kuna shoga yoyote unamfahamu leo mpaka jumapili napokea taarifa zao”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post