CHADEMA YAWATUMBUA KUBENEA,KOMU SAKATA LA KUMSHUGHULIKIA MEYA NA MBOWE


Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imewavua nafasi zote za uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu baada ya kukiri kuwa sauti zilisombaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni za kwao.

Sauti hizo ni zile ambazo wabunge hao wanasikika wakipanga namna ya kumshughulikia Meya wa Ubungo, Boniface Jacob huku Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, akitajwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Oktoba 18,2018, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya wabunge hao kuhojiwa na kamati kuu na kukiri sauti hizo ambazo zilihusisha mazungumzo ya kuashiria utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho ni za kwao.

“Tumewapa adhabu mbalimbali kwa mujibu wa kanuni 6.5 (d) za chama na kamati kuu iliwaita wabunge hao kuja kujibu tuhuma na walifika na kuhojiwa na walikiri mbele ya kamati kuu ya chama kuwa sauti zilizosikika ni zao.

“Tukafikia maamuzi ya kuwapa adhabu mbalimbali pamoja na kuwavua uongozi tuliwapa onyo kali na kuwataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama na kwa watu waliotajwa katika sauti hizo,” amesema Mnyika.

Bethsheba Wambura - Mtanzania

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post