NAY WA MITEGO AITWA BASATA.... AACHIA UJUMBE MTANDAONI

Hapo jana October 17, 2018 msanii Nay wa Mitego alifika kuchukua barua Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Bado Nay hajaweka wazi kile kilichopo ndani ya barua ile ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza hisia zake mara baada ya kutoka Basata, Nay ameandika;


"Unaweza fungwa kila kitu, mikono, mdomo, miguu, kazi na kila kitu but huwezi funga mitazamo na akili za mtu. Itafungwa kwasasa ila muda ukitimia hakuna kitacho shindikana," ameeleza.

Kwa sasa Nay wa Mitego anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Alisema ambao ndio unatajwa kupelekea msanii huyo kuitwa Basata mara mbili ndani ya wiki mbili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post