KAMANDA MAMBOSASA : MO DEWJI BADO HAJAPATIKANA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, LazaroMambosasa amezungumza leo mchana  kuhusiana na tukio la kutekwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mo Dewji ambapo amesema hadi mchana huu taarifa rasmi ni kwamba Mo bado hajapatikana na watekaji bado hawajakamatwa.


Mambosasa amewataka wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambaa mitaani kwamba Mo kapatika akiwa Coco beach kwa kuwa ni za uongo na wala hazijatolewa na ofisi yake.


Amesema jeshi la polisi linaendelea na Opareshen kali kwa kushirikisha mikoa mitatu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana na watekaji wanatiwa Mbaroni

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527