Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) ameongoza harambee ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la darasa katika shule ya Sekondari Itwangi iliyopo katika wilaya ya Shinyanga ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madarasa unaoikabili shule hiyo ambayo sasa ina jumla ya madarasa saba yanayotumiwa na wanafunzi 491.
Mheshimiwa Azza ameendesha harambee hiyo janaAlhamis Oktoba 18,2018 akiwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya tisa ya Kidato cha nne katika shule hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 77 kati yao wasichana ni 37 na wavulana 40.
Katika harambee hiyo Jumla ya mabati 64 yamepatikana ikiwa 25 ni mchango wa mbunge huyo kwa ajili ya upauaji wa jengo la darasa katika shule hiyo ambalo halijapauliwa na linahitaji mabati 56.
Pia pesa taslimu 72,500/= zilipatikana,ahadi shilingi 110,000/=, na misumali kilo 6 vyote vikiwa ni michango kutoka kwa wazazi na wadau waliohudhuria mahafali hayo.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo,Mheshimiwa Azza Hilal aliahidi kuwasomesha na kuwapatia mahitaji yote muhimu wanafunzi watatu wa kike watakaofaulu vizuri masomo ya sayansi na kujiunga kidato cha tano.
"Shule hii iliyoanzishwa mwaka 2007 bado inakabiliwa na ufaulu mdogo kwa wanafunzi wa kike,ni wachache sana wanajiunga na kidato cha tano,mfano mwaka 2013 kati ya wanafunzi 27 waliofaulu kujiunga na masomo ya kidato tano,wasichana ni watatu tu,mwaka 2014 walifaulu 20 lakini wasichana wanne tu walienda kidato cha tano,mwaka 2015 walifaulu nane wote ni wavulana,2016 walifaulu 12, msichana ni mmoja tu na mwaka 2017,walifaulu 13 na wasichana walikuwa wawili tu", alisema Azza.
Aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao na kuepuka vishawishi mbalimbali wanavyokutana navyo huku akiwataka wazazi na walezi kuwapa nafasi watoto wa kike badala ya kuwachukulia kuwa wao ni wa kuolewa tu.
Aidha aliwaasa watoto wa kike kuvaa magauni manne katika maisha yao ambapo gauni la kwanza ni lile la darasa la kwanza hadi kidato cha nne, gauni la pili ni joho,la tatu ni shela endapo wataolewa na gauni la nne ni la ujauzito akibainisha kuwa magauni hayo manne ni ishara ya kujipanga kimaisha.
Mahafali hayo ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Itwangi yamefanyika ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mheshimiwa Azza Hilal aliyezaliwa Oktoba 18 miaka kadhaa iliyopita.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiongoza harambee ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la darasa katika shule ya Sekondari Itwangi.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akilishwa keki kusherehea siku yake ya kuzaliwa Oktoba 18
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikata keki kwa ajili ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Itwangi.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akipokelewa shuleni