KAMANDA SENGA AWATAJA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA BASI LA ARUSHA EXPRESS | MALUNDE 1 BLOG

Monday, October 8, 2018

KAMANDA SENGA AWATAJA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA BASI LA ARUSHA EXPRESS

  Malunde       Monday, October 8, 2018
Na John Walter-Babati.
Watu wanne wamefariki dunia na 11 kujeruhiwa baada ya kupata ajali mbaya ya gari la abiria  walilokuwa wakisafiria kutoka Arusha kuelekea Mbeya mara baada ya dereva kushindwa kulimudu wakati akikata kona kwenye eneo la Mlima Haraa wenye kona kali kata ya Bonga mjini  Babati.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:15 asubuhi ya leo Oktoba 8-2018 katika Bara bara ya Babati-Dodoma ambapo gari la Abiria kampuni ya Arusha Express lenye namba za Usajili T 750- BYQ Scania likitokea Arusha kuelekea mkoani Mbeya lilimshinda dereva huyo aliyefahamika kwa  jinaKennedy Shayo  kurudi upande wa pili wa kulia baada ya kukata kona ya haraka katika eneo lenye mlima na kona nyingi kisha kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi kumi.

Waliofariki ni kondakta wa gari hilo Nassibu Ramadhani  (43) mkazi wa Morogoro, Salvatory Thomas mkazi wa Haraa Babati,Laurent Mwanyabala mkazi wa Mbeya (46) Janefredy Mushi,ni mwanafunzi (21) mkazi wa Galapo Babati.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga  amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba abiria 56 alikimbia kusikojulikana baada ya ajali.

“Tutamtafuta dereva popote alipo kamahatojisalimisha, jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kushindwa kulimudu gari kwenye kona.” alisema Kamanda Senga.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Babati Mrara kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post