ZOEZI LA KUSAJILI WAKAZI WA ZANZIBAR KATIKA MFUMO WA KIELEKTRONI (E-ID CARD) LAANZA


Zoezi la uandikishaji wananchi wa Zanzibari katika mfumo wa kidigitali limeanza rasmi leo Sept 8, 2018 katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja. Ambapo idadi kubwa ya wananchi imejitokeza kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho ya kielektroniki (E-ID CARD). Mapema wiki hii rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alizindua Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki hafla iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Wananchi wakiendelea kuandikishwa.

Mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa.
Wananchi wakingoja foleni ili kuingia katika chumba cha kuandikishwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527