WALIMU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hazina iliyopo Magomeni, Dar es salaam, Patrick Cheche (43) na walimu wenzake wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kupata mitihani na kutoa maudhui ya mitihani hiyo kwa watahiniwa wa darasa la saba isivyo halali.

Akiwasomea hati ya mashtaka leo Septemba 26, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono aliwataja washtakiwa hao kuwa ni mwalimu Laurence Ochien (30), mkazi wa Magomeni Makuti.

Wengine ni mwalimu Justus James (32) Mkazi wa Kimara Mwisho Mavurunza, Nasri Mohammed (32) Mkazi wa Magomeni Makuti.Na Tausi Ally,Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.