Tuesday, September 25, 2018

MWANAMKE AKAMATWA KWA KUISHI NA WAUME WAWILI NDANI YA NYUMBA MOJA

  Malunde       Tuesday, September 25, 2018


Picha: Kutoka mtandaoni (Sio wahusika wa tukio)

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Maurine Atieno mkazi wa kijiji cha Chamgiwadu kaunti ya Migori, amekamatwa na polisi nchini Kenya sambamba na waume zake wawili aliokuwa akiishi nao.

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya majirani kulalamika na kutaka mamlaka husika kumchukulia hatua wakidai kitendo hiko sio sahihi.

Chifu wa eneo hilo David Onyango amesema kwamba mwanamke huyo amekuwa akiishi na waume hao wawili kwa pamoja kama waume zake wa ndoa, kwa muda wa wiki mbili sasa ndani ya nyumba moja.

Ndoa hiyo ya mitala kwa wanaume hao ilitokea pale baada ya Maurine ambaye aliolewa na Robert Ochieng ambaye pia amezaaa naye watoto wawili, kurudi nyumbani akiwa na mpenzi mpya aliyetambulika kwa jina la John Ochola aliyempata kwenye shughuli zake za kuuza samaki huku akimtaja kuwa mteja wake muaminifu, na kuamua kuishi nao wote kwa pamoja.

Chifu huyo ameendelea kwa kusema kwamba wanachunguza ni kwa namna gani watatu hao wamekubaliana kuishi ndani ya nyumba moja, na kwamba ndoa hiyo ya pili ya Maurine na John imethibitishwa na mama wa John ambaye amekiri na kusema kwamba mkwe wao huyo huwa anaenda mara kwa mara kuwatembelea nyumbani kwao.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umesema kwamba hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kuwashtaki, isipokuwa wataangalia namna ya kuwatenganisha watatu hao, ili kuepusha majanga yoyote ambayo yanaweza tokea.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post