BABA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUZAA NA MWANAYE MWANZA

Jacob Shabani (30) mkazi wa kijiji cha Wanzamiso kata ya Igokelo wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanaye mara tatu na kumpa ujauzito.

Akisomewa hati ya mashtaka leo Septemba 25, 2018 mbele ya hakimu Mkuu Mkazi mfawidhi Erick Marley, mwendesha mashitaka wa polisi, Ramsoney Salehe amedai tangu 2015 mshtakiwa alikuwa akiishi kinyumba na mwanaye mwenye umri wa miaka 17.

Amedai binti huyo alipata ujauzito na mimba ikaharibika na mwaka 2016 akapata mimba ya pili na kujifungua mtoto wa kike ambaye alifariki mwaka huo huo na sasa amejifungua mtoto ana wiki mbili na ana ubini wa baba.

Amesema wamebaini jambo hilo kwa kuwa katika kadi hiyo, jina la baba linasomeka, Jacob Shabani.

Salehe ameiileza mahakama kuwa upelelezi umekamilika na shauri hilo kinaweza kusikilizwa na kuna mashahidi wanne na kielelezo cha kadi ya kliniki.

Hakimu Marley ameahirisha kesi hiyo ya jinai namba 74 ya mwaka 2018 hadi Oktoba 2, 2018.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kwa kukosa mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh1milioni.

Na Twalad Salum, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527