RAIS MAGUFULI: SITAPELEKA MAJI CHATO HADI WAJIFUNZE


Rais John Magufuli amesema hatapeleka mradi wa maji Wilaya ya Chato kwa sababu wakazi hao waliharibu mradi wa maji waliopelekewa 1970.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Septemba 8 wakati akizungumza na wananchi wa mji wa Lamadi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa Lamadi, Simiyu.

Alisema miradi mingi ya maji haidumu kutokana na wananchi na viongozi kushindwa kutunza na kuisimamia ipasavyo.

Alitolea mfano katika kijiji cha Chato kilichopelekewa mradi wa maji mwaka 1970 lakini walishindwa kuutunza na mpaka sasa hawana maji. Alisema kamwe hawatapelekewa mpaka wajifunze.

Alisema kuwa yeye hashindwi kupeleka miradi ya maji Chato kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Mwanza,Simiyu na Musoma lakini anafanya hivyo ili wajute na kujifunza umuhimu wa kutunza miundombinu.

"Siwezi kukubali kuona miradi ya maji haidumukwa sababu eti wananchi na viongozi wanashindwa kutambua thamani ya utunzaji wa miradi ya maji na endapo mtashindwa kulinda na kutunza kamwe sitawaletea miradi mingine,”alisema Rais Magufuli

Rais amewataka Viongozi wa Wilaya ya Busega kushirikiana na wananchi ili kutunza mradi wa maji wa Lamadi wenye thamani ya Sh 12.8 bilioni.

Amesema endapo watashindwa kufanya hivyo kamwe hawatapelekewa miradi mingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527