RAIS MAGUFULI AMPIGIA SIMU WAZIRI LUKUVI LIVE NA KUAGIZA KAMISHINA WA KANDA ASIMAMISHWE KAZI


Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa Ardhi William Lukuvi kumsimamisha kazi kamshina wa ardhi kanda ya Mara, aliyemtaja kwa jina la Chawio kwa kosa la kushindwa kushughulikia mgogoro wa ardhi kati ya tajiri mmoja na bibi kizee aitwaye Nyasasi Masike huko Bunda.


Rais ametoa agizo hilo kwa njia ya simu baada ya kukutana na kero hiyo wilayani Bunda alipokuwa akiendelea na ziara yake mkoani Mara ndipo akampigia simu Waziri Lukuvi kupata maelezo ya mgogoro huo.

Katika maelezo yake Mh. Lukuvi alieleza kutambua uwepo wa mgogoro huo na kumwambia Rais kuwa alishatoa maagizo kwa kamishna wa ardhi kanda hiyo na mkuu wa wilaya pamoja na mkoa huo kwa pamoja washughulikie suala hilo.

''Kama ulishatoa maagizo na hajayafanyia kazi huyo kamishna kashindwa kukuheshimu anatakiwa apishe, msimamishe mara moja apishe tuchunguze suala hili la wazee hawa kudhurumiwa viwanja vyao'', amesema Rais.

Awali Bibi huyo (Nyasasi Masike) alimueleza Rais Magufuli kuwa alimuuzia tajiri mmoja eneo la kiwanja chake kwaajili ya kupata fedha ya matibabu na baada ya kupona alikuta kajimilikisha eneo lililokuwa limebaki hivyo kukosa haki yake.

Rais amempatia shilingi laki tano bibi Nyasasi Masike kwaajili ya matumizi yake ya kila siku. Pia Waziri Lukuvi ameahidi kuanzia wiki ijayo atakuwa wilayani Bunda kushughulikia suala hilo na amemwahidi Rais bibi huyo atapata haki yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527