AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI BABATI


Jeshi la polisi mkoa wa Manyara linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Negamsi mjini Babati Mkoani Manyara aliefahamika kwa majina ya Chadema Horay[25] kwa tuhuma za Mauaji.

Tukio hilo limetokea wakati wa ugomvi wa marehemu na mkewe baada ya mke kujenga nyumba bila ya kumshirikisha mume wake ndipo mtuhumiwa alipochukua tofali na kumshambulia marehemu aliyekuwa anabomoa nyumba yenye mgogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema kuwa mauaji hayo yametokea Agosti 4.2018 saa nane mchana na kumtaja marehemu kwa jina la Shadrack Sangu dereva boda boda mkazi wa Negamsii kata ya Bagara mjini Babati.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mji wa Babati Mrara kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527