RAIS MAGUFULI AAHIDI KULIPA MADENI YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA MARINE SERVICE

Rais Dk. John Magufuli ameahidi kulipa madeni ya mishahara ya wafanyakazi wa 'Marine Service' jijini Mwanza ambao wanadai shilingi bilioni 3.7 na atawalipa ndani ya wiki mbili huku akiwaonya kufanya kazi kwa juhudi na ipasavyo.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo akiwa jijini Mwanza kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na Chelezo katika Ziwa Victoria, ambapo ujenzi huo utagharimu shilingi Bilioni 88. 76.

''Mimi nitawapa hizo bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili, sasa ole wenu msifanyekazi tena mtazitapika, nawaambia kabisa huu sio muda wa kubembelezana lazima tubanane kwa sababu tumechelewa'', ameonya Rais Magufuli.

Wafanyakazi hao wanadai malimbikizo ya mishahara ya takribani miezi 27 ambapo Rais Magufuli ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa uendeshaji wa sasa wa Marine Service chini ya Kaimu Mkurugenzi Erick Hamis.

Rais yupo ziarani katika mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527