UJENZI WA MELI MPYA JIJINI MWANZA KUTOA AJIRA KWA WATANZANIA 250

Kaimu meneja wa Kampuni ya Meli (MSCL) Erick Hamis amesema kwamba ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 yenye tani 400 utatoa ajira 250.

Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa meli hiyo mpya na ukarabati wa meli nyingine za MV Viktoria na Mv Butiama na ujenzi wa Chelezo.

Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula amesema kwamba baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama usafiri ulikuwa wa shida.

“Tunatumia fursa hii kukushukuru(Rais Magufuli) kwa jitihada zako na sisi tutakuunga mkono,’’amesema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amesema tukio hilo ni dhahiri kwamba Rais ana dhamira kwa anayoyasema.

Alisema kwamba Rais aliposema anajenga reli kutoka Mwanza alikuwa pia amedhamiria na kwamba miundombinu hiyo itasaidia kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa.

“Wapo watu ambao hawataki kuamini kinachofanyika lakini ukweli ndio huo,’’amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post