Picha : MKUTANO MKUU WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA - UTPC WAFANYIKA JIJINI ARUSHA ... 'WAANDISHI SIYO MAADUI'


Mgeni rasmi,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha Septemba 3,2018 hadi Septemba 4,2018 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog 

******

Rais  wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo ameiomba serikali kuwaangalia waandishi wa habari kwa jicho la tofauti ili kuwalinda kwa kuwa tasnia hiyo sio adui bali ni wadau muhimu wa maendeleo ya nchi. 


Amesema hayo katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania unaofanyika JiJini Arusha,ambapo amesema ndani ya miaka miwili waandishi 57 wamepata matatizo ya kupigwa,kuumizwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi na baadhi kupotea jambo ambalo linaleta woga katika utendaji kazi.

Nsokolo amesema hawawezi kutupia lawama kwa serikali kwa sababu hawajafanya uchunguzi wa kutosha,bali wanaomba kulindwa ili waweze kuchangia maendeleo kupitia kalamu zao.

''Napenda ifahamike pote kuwa waandishi wa habari sio maadui bali ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo vema kushirikiana na sio kuonana maadui,"alisema.

Aidha amemshauri Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuangalia aina ya viongozi anaowateua kutokana na hivi karibuni kujitokeza hadharani baadhi ya kiongozi mmoja kutoa kauli tata kwa mwandishi wa habari aliyepigwa uwanja wa mpira Dar es Salaam.

"Ni wazi tukio hilo la kulaaniwa na halipaswi kufumbiwa macho tunaomba wahusika wachukuliwe hatua maana tunafahamu kabla ya kuingia uwanjani kuna kukaguliwa hivyo huwezi kuingia mtu na silaha,"alisema Nsokolo.

Pia alisema katika mkutano huo iliohudhuriwa na wajumbe 81 toka Klabu 28 Tanzania Bara na Visiwani watatoa Tuzo ya tatu ya Daudi Mwangosi kama ishara ya kuonyesha waandishi hawako salama.

"Lakini tunaomba wafadhili wetu SIDA waangalie jinsi ya kusaidia Klabu ya Dodoma na tutapeleka andiko maalum ili wajengewe ofisi zenye hadhi kulingana na hali ilivyo sasa na kuwapatia mafunzo wanahabari ili wafahamu jinsi ya kuandika habari za viongozi mbalimbali wanaotembelea Dodoma,"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa Balozi wa Sweden Tanzania (SIDA) Ulf Kallsting aliwakumbusha wanahabari kuhakikisha wanaandika habari za utafiti ili kuepuka kuleta shida katika nchi.

"Lakini ili Klabu zenu ziendelee kuwa na vyanzo vingi vya mapato vema mkaongeza idadi ya wanachama,"alisema

Alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Klabu za wanahabari na UTPC na kusema jambo la kuigwa kwani linajenga Demokrasia ya kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao licha ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.

Alisema Wilaya yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo sehemu kubwa inasabishwa na ukosefu wa uelewa wa sheria ya umiliki ardhi na baadhi ya wanasiasa kuitumia kujipatia kura.

"Mimi sitakubali kabisa kuachia wanasiasa wajinufaishe na migogoro hii lazima nibadilishe badala ya ardhi kuwalaana bali iwe baraka hasa Halmashauri ya Meru, na hili nimeanza kuzungumza na viongozi wadini tusaidiane kulimaliza,"alisema.

Habari imeandaliwa na Vero Ignatus- Malunde1 blog Arusha. 


Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili hotuba ya Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting.
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC),Deogratius Nsokolo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC).
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati wa wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC).
Jerry Muro akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kushoto ni Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji,Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo na Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akishikana mkono na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC),Deogratius Nsokolo.
Wajumbe wa jopo la Tuzo ya Daudi Mwangosi wakiwa ukumbini.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro.
Afisa Programu,Mafunzo, Utafiti na Uchapishaji wa UTPC Victor Maleko akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za UTPC
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC wakiwa ukumbini
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) Kadama Malunde, na Katibu wa wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Ali Lityawi wakiwa ukumbini.
Viongozi wa klabu za waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa klabu mpya ya waandishi wa habari mkoa wa Songwe (wa tatu kutoka kushoto).
Picha ya pamoja meza kuu na wenyeviti wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na makatibu wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na waweka hazina wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC
Picha ya pamoja meza kuu na wajumbe wa jopo la Tuzo ya Daudi Mwangosi 
Picha ya pamoja meza kuu na wafanyakazi wa UTPC
Kushoto ni Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting,Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji na kurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan wakifurahia jambo
Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akiteta jambo na Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji.
Mwenyekiti wa SPC,Kadama Malunde akipiga selfie na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan,Makamu wa Rais UTPC,Jane MihanjiRais wa UTPC,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting na rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo.

- Picha zote na Kadama Malunde na Emmanuel Msumba - Malunde1 blog & Msumba News blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post