OXFAM YAWAKUTANISHA WADAU WA TAASISI ZA KIRAIA NCHINI KUJADILI KUHUSU UCHIMBAJI WA MAFUTA,GESI NA MADINI JIJINI DAR

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Christopher Ngubiagai akizungumza juu ya uziduaji wa gesi hasa kuhusiana na uwazi wa mikataba na ukusanyaji wa mapato katika Wilaya ya Kilwa wakati wa  mjadala uliloandaliwa na  Oxfam Tanzania uliowahusisha wadau kutoka  sekta mbalimbali kuhusiana na uwazi wa  mikataba na ukusanyaji wa mapato sekta ya Gesi, Mafuta na Madini.
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la kimataifa Oxfam Tanzania Bi. Betty Malaki, akitoa neno la ufunguzi wakati wa mjadala uliloandaliwa na  Oxfam Tanzania uliowahusisha wadau kutoka sekta mbalimbali kuhusiana na uwazi wa  mikataba na ukusanyaji wa mapato sekta ya Gesi, Mafuta na Madini.
Bw. Amani Mhinda kutoka HakiMadini akielezea kwa undani kuhusu umuhimu wa kuweka wazi mikataba ya mafuta,gesi na madini kwa wananchi ambayo Serikali inatiliana saini na makampuni ya Uchimbaji.
Meneja wa Kampeni Kutoka Shirika la kimataifa la Oxfam Tanzania Bi. Jovitha Mlay akielezea faida mbalimbali za kuweka wazi Mikataba ikiwa ni pamoja na wadau wengine kufahamu taarifa zilizopo kwenye mikataba.
Bw. Albert Mhombeki Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi (Aliyevaa miwani) akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa jadala uliloandaliwa na  Oxfam Tanzania uliowahusisha wadau kutoka
sekta mbalimbali kuhusiana na uwazi wa  mikataba na ukusanyaji wa mapato
sekta ya Gesi, Mafuta na Madini.
 Mmoja wa washiriki katika mkutano huo Bi. Betty akiuliza swali 
Bw. Godfrey Jafary Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilwa akitoa ufafaniuzi wa mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa mkutano huo.
Bi. Maureen Mboka ambaye ni Afisa utafiti na uchambuzi kutoka asasi ya kiraia ya TGNP, akielezea maswala mbalimbali yanayohusiana na uhusiano kati ya uhusiano kati ya ukusanyaji wa mapato yanayotokana na Uziduaji na jinsia.
Bw. Sifael Msovu Meneja mapato kutoka TPDC akiongea wakati wa mkutano huo ambapo alisema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa sekta ya Madini nchini ikiwa lengo ni kuendeleza sekta hiyo.
Mmoja wa waandishi wa Habari akitaka ufafanuzi wa jambo kuhusiana na Gesi wakati wa mkutano huo.
Mraghbishi Farida Mpela akiuliza maswali na kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika maswala ya uchimbaji wa Gesi
Bi. Theo Kasiga Afisa Programu msaidizi kutoka NRGI akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika mkutano huo.
Mkutano ukiwa unaendelea
Picha zote na Fredy Njeje



Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kiraia nchini walikutana  jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa siku moja uliolenga kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na sekta ya uchimbaji wa mafuta, gesi na madini.

Moja ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano ni kuhusu umuhimu wa kuweka  wazi mikataba ya mafuta, gesi na madini kwa wananchi ambayo Serikali inatiliana saini na makampuni ya uchimbaji.




Akizungumza wakati wa mkutano huo, Meneja wa kampeni kutoka shirika lisilo la kiserikali, Oxfam Tanzania, Bi. Jovitha Mlay alizitaja faida mbalimbali za kuweka wazi mikataba hiyo kwa wananchi.

Moja ya faida hizo ni kuwawezesha wananchi pamoja na wadau wengine kufahamu taarifa zilizomo kwenye mikataba pamoja na kufahamu kiasi gani Taifa linafaidika kutokana na gesi asilia, mafuta na madini.

"Serikali na makampuni ya uchimbaji yana wajibu kisheria kuweka wazi taarifa zilizomo kwenye mikataba ili kuwawezesha wananchi kufahamu kinachokubaliwa baina ya pande mbili," alisema.

Nae kwa upande wake, meneja wa mapato kutoka kampuni ya TPDC, bwana Sifael Msovu alisema kwamba serikali iko tayari kushirikiana na wadau wa sekta ya madini nchini ikiwa lengo ni kuiendeleza sekta hiyo.

Pia alisema suala la kuweka wazi taarifa zilizomo kwenye mikataba ya uchimbaji ni suala la kisheria, na akasisitiza kwa serikali itahakikisha makampuni yote yanaweka wazi mikataba yao ili kuwawezesha wananchi kufahamu taarifa hizo.



"Tayari sheria imeshatungwa na imeshapitishwa bungeni ambayo inaitaka serikali pamoja na mashirika ya uchimbaji kuweka wazi taarifa za mikataba kwa wananchi," alisema.

Pia aliongeza, sheria inaeleza kwamba sio kila taarifa zilizomo kwenye mikataba zinatakiwa ziwekwe wazi kwa wananchi. Baadhi ya taarifa zilizomo kwenye mikataba ni za kibiashara hivyo haziwezwi kuwekwa wazi kama ambavyo sheria inaelekeza,"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527