Picha : BENKI YA NMB KAHAMA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA ' WANACHAMA WA BUSINESS CLUB'


Benki ya NMB tawi la Kahama mkoani Shinyanga, imekutana na wateja wake ambao ni wafanyabiashara (Business Club), kwa ajili ya kujadili na kuzitatua changamoto ambazo huwa zinawakabili hasa kwenye ukopaji wa mikopo ili kuboresha huduma kwao na kuwainua kiuchumi.


Kikao hicho kimefanyika leo Septemba 14, 2018 wilayani Kahama kwenye ukumbi wa Kapaya, ambapo jumla ya wanakikundi wa klabu 250 wamekutana.

Mgeni Rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha.

Awali akizungumza katika kikao hicho,Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Leon Ngowi amesema lengo la kikao hicho ni kujadili changamoto ambazo huwa zinawakabili wafanyabiashara hao ambao ni wateja wa Benki hiyo ili kuboresha huduma kwao na kuendelea kuitumia benki kukopa fedha ili kuwainua kiuchumi.

“Ndani ya kikao hiki pia tutafahamiana, na mtapewa elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kupanua wigo wa biashara zenu, na namna ya kuweza kulipa marejeshobila kukwama pale unapokuwa umechukua mkopo,”alisema Ngowi

“Na sisi kama Benki ya NMB, changamoto ambazo mtaziainisha hapa tutazichukua na kwenda kuzifanyia kazi, ili kuendelea kuboresha huduma kwenu kwa  sababu benki yetu inajali sana wateja wake, na hatutataka kuwapoteza bali tunataka mtajirike kupitia mikopo ya NMB,”aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Klabu hiyo ya NMB Azan Salumu, alipaza kilio cha wafanyabiashara hao kuwa wanaomba riba ipunguzwe ili wafanyabiashara wengi waweze kujitokeza kuchukua mikopo Benki pamoja na kuweza kurejesha marejesho kwa wakati bila ya kukwama.

Kwa upande wake mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, aliipongeza benki hiyo kwa ubunifu walioufanya wa kukutana na wateja wao ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Aidha aliiomba benki hiyo ipunguze riba za mikopo kwa wateja wao ili wapate kuongeza wateja wengi ambao watakuwa wakirejesha kwa wakati na kutofirisiwa mali zao.

Pia alitoa rai kwa wafanyabiashara wote wilayani humo, kujenga tabia ya kulipa kodi ili kuiongezea mapato serikali, fedha ambazo zitasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwamo na kuboresha miundombinu ya barabara ambayo itawarahishia kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Ester Derefa, ambaye anafanya biashara ya kusindika viungo vya chakula, aliipongeza benki hiyo kumuinua kiuchumi ambapo mwaka 2015 alikopa shilingi 300,000 kuanza biashara hiyo, lakini mpaka sasa ana mtaji wa shilingi Milioni 10.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Leon Ngowi, akizungumza kwenye kikao cha wafanyabiashara ambao ni wateja wa benki hiyo na kusema lengo lake ni kujadili changamoto ambazo huwa zinawakabili wafanyabiashara ili kuboresha huduma kwao na kuendelea kuitumia benki kukopa fedha ili kuwainua kiuchumi - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mwenyekiti wa wafanyabiashara Business Club wa Benki ya NMB Azan Salumu akiomba riba ipunguzwe ili wafanyabiashara wengi waweze kujitokeza kuchukua mikopo Benki, pamoja na kuweza kurejesha marejesho kwa wakati bila ya kukwama.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliwataka wafanyabiashara wote wilayani humo kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi bali wajitokeze ili kuchangia ongezeko la mapato serikalini, fedha ambazo zitasaidia kuleta maendeleo wilayani humo ikiwamo na ujenzi wa miundombinu mizuri ya barabara ambayo itasaidia biashara zao kufanyika kwa ufanisi.

Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani Kahama Deo Marisho akitoa elimu ya mlipa kodi na kubainisha kuwa kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato serikalini na kuwataka pia pale wanapouza bidhaa zao watoe risiti.

Mtaalamu wa mafunzo kutoka EIB Fathili Boniphace akitoa elimu kwa wafanyabiashara hao namna ya kutumia fursa kupanua wigo wa biashara zao na hatimaye kukua kiuchumi.

Meneja wa benki ya NMB Tawi la Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akitoa salamu kwa wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama ambao ni wateja wa benki hiyo wilayani humo.

Meneja wa Benki ya NMB kutoka Bukombe George Fundi akitoa salam kwa wafanyabiashara wa wilayani Kahama, ambao ni wateja wa benki hiyo.

Wafanyabiashara wa Kahama ambao ni wanachama wa Business Club tawi la Kahama wakiwa kwenye kikao chao na benki hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwamo kupewa elimu ya mlipa kodi, namna ya kumudu marejesho ya mikopo,kupanua wigo wa biashara pamoja na kutatuliwa kero zinazowakabili hasa kupunguziwa riba ya mikopo.

Wafanyabiashara wakiendelea na kikao chao na wadau wao wa benki ya NMB Tawi la Kahama katika ukumbi wa Kapaya wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwataka pia wafanyabiashara hao kuwa wanatunza kumbukumbu ya biashara zao.

Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa Kapaya wilayani Kahama.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Magharibi Leon Ngowi akielezea namna benki hiyo inavyowajali wateja wake ambapo imeweza kupunguza riba kwa wakopaji wa kati kutoka asilimia 21 mpaka 19, mikopo ya chini kutoka asilimia 23 mpaka 21, huku akiahidi kuendelea kutatua changamoto zingine ambazo zinawakabili wateja wao, ili waendelea kufurahia huduma katika benki hiyo.

Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikendelea kwa kusikiliza elimu mbalimbali kutoka kwa wataalamu ikiwamo ya mlipa kodi na namna ya kurejesha marejesho ya mikopo bila kukwama pamoja na kupanua wigo wa biashara kwa kutumia fursa.

Kikao kikiendelea.

Wafanyabiashara wakiwa ukumbini



Awali wafanyabiashara wakisimama kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kuwafungulia kikao hicho ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiangalia baadhi ya bidhaa kutoka kwa wafanyabishara ambao ni wanachama wa Business Club kutoka tawi la Benki ya NMB Kahama ambao walikopa mikopo na kuweza kuinuka kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiendelea kukagua bidhaa.

Mfanyabiashara Ester Derefa akionyesha bidhaa zake za kisindika viungo vya chakula, ambapo awali alikopa mkopo Benki ya NMB Shilingi 300,000, lakini mpaka sasa ana mtaji wa Shilingi Milioni 10.

Mwandishi wa habari wa ITV Mkoani Shinyanga Frank Mshana akiangalia bidhaa za mfanyabiashara Ester Derefa.

Bidhaa zikiendelea kuonyeshwa.

Awali Meneja wa NMB Tawi la Kahama Richard Kilenga akikaribisha wageni na wafanyabiashara wa Business Club kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akigawa vyeti kwa wafanyabiashara 15 ambao wamefanya vizuri ambapo Brayani Gervas akipokea cheti kwa niaba ya Kampuni ya Kahama Oil Mil.

Maimuna Misana kutoka Sefaha Interprises ambao wanahusika na kuongeza thamani ya mazao akipokea cheti cha pongezi kutoka Benki hiyo ya NMB.

Vyeti vya Pongezi vikiendelea kutolewa.

Zoezi la kugawa vyeti vya pongezi likiendelea

Vyeti vya Pongezi vikiendelea kutolewa.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, akisalimiana na wafanyabiashara wakati akiondoka kwenye kikao hicho cha NMB na wateja wao, cha kuboresha huduma bora kwa wateja wake.

Viongozi wa Benki ya NMB, pamoja na mkuu wa wilaya Anamringi Macha wakipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara washindi 15 kutoka Benki ya NMB tawi la Kahama.

Viongozi wa Benki ya NMB, pamoja na mkuu wa wilaya Anamringi Macha wakipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara washindi 15 kutoka Benki ya NMB tawi la Kahama.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post