RAIS MAGUFULI ATEMBELEA SHULE ALIYOSOMA MWL NYERERE

Leo Septemba 5, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara na kutembelea shule ya msingi Mwisenge aliyosoma Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwaahidi kuwapatia kiasi cha fedha Milioni 2o ndani ya wiki mbili na kutaka fedha hizo zitumike kukarabati shule hiyo.

Mbali na ahadi hiyo Rais Magufuli ametoa papo kwa papo kiasi cha fedha Shilingi Milioni Moja kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi pamoja na macho ili washerekee fedha hiyo na walimu wao.

Aidha Rais amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii kwani Serikali inawawependa na kuwajali.

Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post