LIPULI FC, MBEYA CITY SAFI, MTIBWA NA AZAM ZABANWA


Mchezo wa Lipuli Fc dhidi ya Alliance Academy

Ratiba ya ligi kuu Tanzania bara imeendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti ambapo vigogo wameendelea kubanwa kupata alama tatu.

Azam Fc imepata sare ya pili kanda ya ziwa baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Biashara United ya mkoani Mara baada ya kupata sare dhidi ya Mwadui Fc wikiendi iliyopita. Nayo Mtibwa Sugar imepoteza mchezo wake dhidi ya Ndanda Fc kwa mabao 2-1 mkoani Mtwara baada ya kuambulia sare ya bila kufungana na Lipuli Fc wikiendi iliyopita.

Mbeya City imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ni ushindi wake wa pili mfululizo msimu huu, baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 wikiendi iliyopita dhidi ya Alliance Academy ya Mwanza.

Lipuli Fc ikicheza mechi ya pili mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani wa Samora imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance Academy baada ya kutoka sare na Mtibwa Sugar katika mchezo wa wikiendi iliyopita.

Matokeo ya mchezo mwingine, Mwadi Fc imetoka sare ya 1-1 na JKT Tanzania katika uwanja wake wa nyumbani na mchezo wa mwisho wa leo, Yanga itwakaribisha Coastal Union katika uwanja wa taifa, mchezo ambao utaanza saa moja usiku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post