HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA YANGA LEO

Leo 30.9.2018 ni siku ya pambano la watani wa jadi kati ya SImba na Yanga mechi ya ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL.
Kuelekea mchezo huo tayari makocha wa timu hizo wameonekana kuwa na vikosi wanavyoviandaa kwaajili ya mechi ya Leo.
Kocha Patrick Aussems kwa siku za Karibuni akiwa na Kikosi cha Simba amekuwa akitumia Kikosi hiki kikionekana ndicho anachokiandaa kwaajili ya Pambano dhidi ya Yanga.
Golini Aishi Manula akisaidiwa na mabeki wa kulia na Kushoto Shomari Kapombe na Mohammed Hussein Zimbwe.
Mabeki wa Kati Erasto Nyoni na Pascal wawa ambao toka ligi kuu imeanza wamekuwa wakicheza kama beki pacha.
Eneo la kiungo Jonas Mkude, Cletous Chama huku James Kotei akicheza kama namba 7 ambaye anasidia zaidi eneo la katikati ya uwanja huku winga ya Kushoto Shiza Kichuya akionekana kupewa nafasi katika kikosi cha Simba.
Washambuliaji : Emmanuel Okwi na Meddie Kagere ndiyo washambuliaji ambao wamekuwa wakionekana kuanza kwenye kikosi kinachoandaliwa kumuua Yanga leo 30.9.2018.Kukipata Kikosi kwa wakati cha Simba hakikisha Umelike Ukurasa wetu wa Facebook BONYEZA HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post