MHADHIRI WA UDSM NA MTANGAZAJI RADIO ONE AFARIKI DUNIA


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Dk Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Septemba 16, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa.

Mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One alikuwa akisumbuliwa na kiharusi, msiba upo nyumbani wake Makongo, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuacha kazi ya utangazaji, Bingi alijiunga na UDSM na alipohitimu masomo aliajiriwa chuoni hapo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.