Friday, August 24, 2018

TANAPA YATENGA BILIONI 3.9 KUENDELEZA HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI NA KUWA HIFADHI ZA TAIFA

  msumbanews       Friday, August 24, 2018Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana kwenye mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha  wageni i katika eneo la Nyungwe wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.

Baadhi ya mafuvu ya wanayamapori katika Pori la A kiba la Burigi katika eneo la Nyungwe. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU) .
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA .

Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa. 

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa akihitimisha bajeti ya Wizara mwezi Mei mwaka huu Bungeni mjini Dodoma. 

Ofisa Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga wakati alipotembelea mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo. 

Alitaja fedha hizo kuwa zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa kupandisha hadhi mapori  Damian Saru, Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo. 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post