Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUBAKA MTOTO WAKE

Mkazi wa Stendi mpya, Mugumu, Nyamhura Werema (35)amepandishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka(12).


Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa polisi, Paskael Nkenyenge amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka huu.


“Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” amesema


Amesema Upelelezi haujakamilika na mshitakiwa amekana shitaka. Mshtakiwa amenyimwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com