POLISI WAZUNGUMZIA TUKIO LA MWANDISHI WA HABARI KUPIGWA NA ASKARI POLIS | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 10, 2018

POLISI WAZUNGUMZIA TUKIO LA MWANDISHI WA HABARI KUPIGWA NA ASKARI POLIS

  Malunde       Friday, August 10, 2018
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa mwandishi wa habari wa Wapo Redio, Sillas Mbise.

Mbise anadaiwa kushambuliwa na polisi juzi Agosti 8, 2018 wakati wa mchezo kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana.

Video za tukio hilo zimesambaa katika mitandao ya kijamii, zikimuonyesha Mbise akishushiwa kipigo na polisi.

Akizungumza leo Ijumaa Agosti 10, 2018 Mambosasa amesema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha hizo za video.

Amesema hiyo inakwenda sambamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Amesema mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post