PAPA FRANCIS ATAKIWA KUJIUZULU


,Kiongozi wa ngazi za juu wa zamani wa Vatican amemtaka kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ajiuzulu wadhifa wake akimshutumu kuwa alikuwa akijua kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya kadinali maarufu wa Marekani, Theodore McCarrick, miaka mitano iliyopita kabla ya kukubali kujiuzulu kwake mwezi uliopita.

Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano aliweka wazi hoja yake katika barua ya kurasa 11 iliyochapishwa Jumapili kwenye Gazeti la Taifa la Kikatoliki pamoja na tovuti nyingine ya kihafidhina, LifeSiteNews.

Vigano, mwenye umri wa miaka 77, amesema alimwambia Papa mwaka 2013 kwamba Kardinali McCarrick alikuwa anadaiwa kuhusika na unyanyasaji wa kijinsia wa makuhani wa ngazi za chini.

Papa aliyemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Ireland ametupilia mbali madai hayo dhidi yake wakati akirejea mjini Roma, Italia
Theme images by rion819. Powered by Blogger.