ORODHA YA MIJI 10 BORA KUISHI DUNIANI 2018...MIJI 10 ISIYO BORA KUISHI 2018

Mji mkuu wa Austria, Vienna, umeorodheshwa kuwa mji bora zaidi kwa watu kuishi duniani, na kuchukua nafasi ya mji wa Melbourne wa Australia ambao umeongoza kwa miaka mingi.

Mji wa Harare, Zimbabwe ni miongoni mwa miji ambayo haivutii kwa watu kuishi duniani.

Ni mara ya kwanza kwa jiji la bara Ulaya kuongoza kwenye orodha hiyo ya kila mwaka ambayo huandaliwa na Kitengo cha Uchunguzi cha Jarida la Economist.

Utafiti huo uliorodhesha miji 140 duniani kwa kufuata vigezo mbalimbali vikiwemo uthabiti wa kisiasa na kijamii, visa vya uhalifu, elimu na kupatikana kwa huduma bora ya afya.

Katika utafiti huo, jiji la Manchester ndilo lililoimarika zaidi miongoni mwa miji ya Ulaya ambapo jiji hilo lilipanda hatua 16 hadi nafasi ya 35.

Jiji hilo limo mbele ya London kwa hatua 13, ambalo ndilo pengo kubwa zaidi kwa miji hiyo miwili kwenye orodha hiyo tangu kuanza kuandaliwa kwa orodha hiyo miongo miwili iliyopita.

Jarida la Economist limesema kuimarika kwa Manchester ni kwa sababu ya kuimarishwa kwa usalama.

'Ukakamavu'

Utafiti huo ulikosolewa mwaka jana kwa kuushusha hadhi mji wa Manchester baada ya shambulio la Manchester Arena ambapo watu 22 waliuawa.

Mwaka huu, mhariri wa utafiti huo Roxana Slavcheva amesema jiji la Manchester "limenyesha ukakamavu na kujikwamua kutoka kwa shambulio hilo la kigaidi ambalo lilikuwa imetikisa uthabiti wake.

Bi Slavcheva amesema usalama pia umeimarika katika miji kadha ya Ulaya magharibi.

Kuongoza kwa Vienna ni iashara ya kurejea kwa utulivu kiasi katika maeneo mengi ya Ulaya.Melbourne ilikuwa awali imeongoza kwa miaka saba mtawalia

Kwa mujibu wa utafiti huo, karibu nusu ya miji imeimarika katika mwaka mmoja uliopita.

Melbourne, ambao kwa sasa ni mji wa pili duniani kwenye orodha hiyo, ilikuwa imeongoza kwa miaka saba mfululizo.

Majiji mengine mawili ya Australia pia yamo kwenye orodha ya kumi bora mwaka huu: Sydney na Adelaide.

Upande ule mwingine, mji mkuu wa Syria, Damascus ambao umeathiriwa sana na vita ndio usiopendwa zaidi na watu duniani ukifuatwa na Dhaka nchini Bangladesh na Lagos nchini Nigeria.

Economist wanasema kwamba uhalifu, machafuko, ugaidi na vita vilichangia sana katika kuorodheshwa chini kwa miji iliyoshika mkia.

Miji bora zaidi kuishi duniani 2018

1. Vienna, Austria

2. Melbourne, Australia

3. Osaka, Japan

4. Calgary, Canada

5. Sydney, Australia

6. Vancouver, Canada

7. Tokyo, Japan

8. Toronto, Canada

9. Copenhagen, Denmark

10. Adelaide, Australia
Unaweza kusoma pia:

Miji isiyo bora kuishi duniani 2018

1. Damascus, Syria

2. Dhaka, Bangladesh

3. Lagos, Nigeria

4. Karachi, Pakistan

5. Port Moresby, Papua New Guinea

6. Harare, Zimbabwe

7. Tripoli, Libya

8. Douala, Cameroon

9. Algiers, Algeria

10. Dakar, Senegal
Miji ghali zaidi kwa watu wa nje kufanyia kaziJiji la Hong Kong ni miongoni mwa majiji yaliyo na msongamano mkubwa zaidi wa nyumba duniani

Miezi miwili iliyopita, kulitolewa ripoti nyingine iliyoonyesha miji ambayo ni ghali zaidi kwa watu wa nje kufanyia kazi duniani ambapo Hong Kong iliongoza.

Mji mkuu wa Angola, Luanda uliongoza mwaka jana kwa mujibu wa utafiti huo wa Mercer.

Utafiti huo uliangazia mambo mengi yakiwemo makazi, nguo na bei ya vitu vingine kama vile mkate na bia. Kuna pia tiketi za kutazama filamu kumbi za sinema, bei ya lita ya maji, bei ya kikombe cha kahawa, bei ya petroli na bei ya lita ya maziwa, pamoja na usafiri.

Mji wa Tokyo ni wa pili mwaka huu ukifuatwa na Zurich nchini Uswizi na Singapore. Seoul nchini Korea Kusini ulikuwa wa tano, ikiwa na maana kwamba majiji manne kati ya matano ghali zaidi yalikuwa ya kutoka bara asia.

Katika miji kumi ya 10, miji iliyofuata ni Luanda, Shanghai, N'Djamena, Beijing na Bern.

Mji nafuu zaidi kwa wageni kufanyia kazi ulikuwa Tashkent, ukifuatwa na Tunis na Bishkek.

Mercer hutumia New York kama kigezo.Jiji la Hong Kong lina majumba mengi marefu

London ilipanda hatua 10 hadi nafasi ya 19 kwenye Orodha hiyo.

Miji mingi ya Ulaya pia ilipanda kutokana na kudhoofika kwa sarafu zake dhidi ya dola ya Marekani pamoja na mfumko. Frankfurt ilikuwa nafasi ya 68 na Berlin 71 nao mji wa Munich nafasi ya 57.
Chanzo -BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527