Thursday, August 30, 2018

MKUU WA MKOA AITULIZA FAMILIA YA MWANAFUNZI ALIYEUAWA KWA KIPGO.......MKUU WA SHULE, MAKAMU WAKE NA AFISA ELIMU KATA WASIMAMISHWA KAZI

  Malunde       Thursday, August 30, 2018
Kifo cha mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta Siperius Eradius aliyedaiwa kuuawa na mwalimu wake kimeondoka na walimu watatu huku familia ya marehemu ikikubaliana na uchunguzi ambao haujawekwa wazi.


Akizungumza leo Alhamisi Agosti 30, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti baada ya kutembelea shule hiyo, amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba awasimamishe kazi walimu watatu ili wachunguzwe kama walitekeleza majukumu yao.


Waliosimamishwa ni Renatha Izidory aliyekuwa mwalimu mkuu na msaidizi wake Sunday Elisha na ofisa elimu wa Kata ya Kibeta, Hashimu Mponda.


Mkuu huyo wa mkoa pia amekwenda kwa familia ya marehemu na kubainisha kuwa familia hiyo imekubaliana na matokeo ya uchunguzi wa pili wa kifo cha mwanafunzi huyo uliofanywa na madaktari kutoka nje ya Mkoa wa Kagera.


Awali, familia hiyo ilisusia mwili wa mwanafunzi huyo baada ya uchunguzi uliotolewa na mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa Mkoa wa Kagera, Dk John Mwombeki kueleza kuwa mwili wake ulikutwa na alama zinazoonyesha alipigwa siku kadhaa kabla ya kukutwa na umauti.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post