POLISI WASEMA MTAWA ALIJIRUSHA MWENYEWE GHOROFANI,HAKUSUMWA NA MTU

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema picha za kamera za CCTV walizonazo zinamuonyesha aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Bugando, Mtawa Suzan Batholomeo (48) akipanda kwenda ghorofani na kujirusha.


Hivyo ameitaka jamii kuacha kusambaza uzushi kuwa huenda mtawa huyo aliuawa.


Mtawa huyo alifariki akidaiwa kujirusha gorofani Agosti 28 mwaka huu.


Akizungumza leo Agosti 30, Shanna amesema: “Tuna vithibitisho kamili ikiwamo kamera za CCTV zikimuonyesha Mtawa huyo akipanda ghorofani na wakati akijirusha, hivyo hayo yanayosemwa kwenye mitandao wasiyaamini sana.”


Ameutaka umma kuacha kuamini tetesi za mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo.


Pia, Shanna amesema wanaendelea kufanya uchunguzi na hivi karibuni ataita vyombo vya habari ili kujibu maswali ya wananchi waliyokuwa wakijiuliza kuhusu kifo cha Mtawa huyo.


Kuhusu mtawa huyo kugawa mali zake kwa ndugu siku chache kabla ya kifo chake, Shanna amesema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwani linaweza kuharibu uchunguzi unaoendelea.


Siku chache kabla ya kifo chake, ofisi ya mtawa huyo aliyekuwa mkurugenzi wa fedha ilikuwa akikabiliwa na upotevu wa zaidi ya milioni Sh300 .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post