Wednesday, August 8, 2018

MKUTANO WA CHADEMA WAPIGWA MABOMU....MBUNGE,MWANDISHI WA HABARI MBARONI

  Malunde       Wednesday, August 8, 2018

Mkutano wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Turwa, (Chadema) umeshindwa kufanyika baada ya polisi kuwatanya kwa mabomua ya machozi wafuasi wa vyama vya upinzani waliohudhuria mkutano huo.

Wakati huo huo, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na wananchi wengine zaidi ya 10 wamekamatwa na polisi akiwamo mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Sita Tuma ambaye pia amekamatwa.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Henry Mwaibambe hakupatikana kuzungumzia kamatakamata hiyo wala simu yake ya mkononi haikupokewa.

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alitarajiwa kuhutubia mkutano huo.

Akizungumzia tukio hilo, katibu wa Chadema mkoa wa Mara, Chacha Heche amedai kwamba chama chake kimezuiwa kufanya mkutano wa kampeni kuanzia leo Agosti 8, 2018 hadi Agosti 11.

Hata hivyo Heche amesema chama hicho hakikupewa barua rasmi ya kuzuiwa kufanya mkutano huu wa kampeni.

“Walikuja asubuhi kwenye ofisi za chama wakitaka tusifanye mkutano lakini hakukuwa na sababu ya msingi ya sisi kutofanya mkutano,” amesema.

Hata hivyo Zitto amesema wataendeleza kampeni hizo kwa kushiriki mikutano ya kampeni ya NCCR-Mageuzi.

Kadhalika Zitto amesema polisi wamemzuia kumuona Esther kituo cha polisi anamoshikiliwa.

Na Waitara Meng'anyi, Mwananchi. 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post