Wednesday, August 8, 2018

RAIS ATISHIA KUWAUA POLISI AKIDAI HAWANA MAANA NA MZIGO KWA JAMII"

  Malunde       Wednesday, August 8, 2018

Askari polisi
Rais Rodrigo Duterte 

Rais Rodrigo Duterte  wa nchi ya Ufilipinoametishia kuwaua makumi ya maofisa wa Jeshi la Polisi la Ufilipino (PNP) ambao wako chini ya uchunguzi kwa uhalifu katika hotuba iliyojaa dharau akilenga wahalifu ndani ya jeshi hilo.

Baada ya kuwapeleka maofisa wa polisi 102 eneo la MalacaƱang, Duterte, rais mwenye maneno ya ufedhuli, Jumanne aliwashambulia akisema “hawana maana” (na) mzigo kwa jamii.”

Majina ya maofisa wengi wa polisi waliopelekwa kwa Duterte yako chini ya uchunguzi kwa makosa makubwa ya uhalifu yakiwemo ya ubakaji, kuteka, kupotosha na kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya.

Wengine wanalalamikiwa kwa uongozi wa kizembe kama vile kutoweka kazini bila idhini wala likizo na kushindwa kuhudhuria kwenye majukumu ya kimahakama.

Duterte aliwaonya maofisa hao kwamba ikiwa wataendelea na vitendo vyao vya uhalifu itakuwa vema wakiuawa.

"Kama ninyi mfanyavyo, ni rahisi kuua mtu. Ni suala la kumnyatia na kumtwanga risasi mgongoni, kisha unatoweka kimyakimya," alisema.

Vitisho hivyo vilivyofikia kiwango cha juu ni katika juhudi za rais kuhakikisha anaendeleza mtindo wake wa kutia chumvi.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Duterte alitoa wito wa kulifumua jeshi la polisi katika kipindi ambacho mfanyabiashara wa Korea Kusini inadaiwa aliuawa na maofisa wa polisi mafisadi.

"Jisafisheni. Pitieni upya matukio yenu. Nipeni orodha ya maofisa wahuni,” alisema Duterte.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post