Picha : RAIS MAGUFULI ASHINDWA KUJIZUIA, AMWAGA MACHOZI AKIAGA MWILI WA KING MAJUTO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi wakati alipokuwa akiaga mwili wa aliyekuwa msanii nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2018.


Rais Magufuli alifika Karimjee na kujumuika na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na waombolezaji wengine katika kuaga mwili wa nguli huyo aliyefariki dunia jana Jumatano, majira ya saa 2 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili alipokuwa akitibiwa.

Mwili wa Mzee Majuto umesafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga ambako atazikwa kesho Ijumaa, Agosti 10, 2018 mchana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527