MTOTO WA LOWASSA AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE MONDULI


 Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa Fred Lowassa ni miongoni mwa wanachama watano wa Chadema waliochukua fomu za kugombea ubunge jimbo la Monduli mkoani Arusha.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga alijiuzulu na kujivua uanachama wa Chadema na kuhamia CCM.

Katibu wa Chedema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa akizungumza na Mwananchi leo Agosti 9 alisema Fred amechukua fomu na kurejesha.

Golugwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, aliwataja wagombea wengine ni Cecilia Ndosi ambaye ni Mwenyekiti Baraza la Wanawake wa Chadema mkoa Arusha na Diwani viti maalum.

Amesema wengine ni Yona Laizer, Lobulu Kivuyo na Eric Ngwijo.

Amesema wagombea hao watapigiwa kura za maoni katika kikao kitakachofanyika Jumamosi kata ya Migungani wilaya ya Monduli.

“Kikao hicho kitaratibiwa na ofisi ya Kanda ya kanda ya kaskazini na baadaye majina kupelekwa kamati kuu,” amesema.

Golugwa amesema katika jimbo la Korogwe vijijini mgombea mmoja amejitokeza ambaye ni Amina Saguti.

Wengine waliochukua fomu kwa upande wa Korogwe Vijijini lakini hawakurejesha hadi ulipofika mwisho wa kurudisha fomu ni Aroan Mashuve na Dafi Dafi.

Golugwa amesema kikao cha kumjadili mgombea huyo kitafanyika Jumapili Korogwe.
Na Mussa Juma,mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527