MWANAFUNZI APANDISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA BODABODA


Watu wawili akiwamo mwanafunzi wa Sekondari ya Mugumu Kurwa Daniel (19) na raia wa kawaida Paulo Marwa (30) wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti mkoa Mara wakidaiwa kuiba pikipiki.

Mwendesha mashtaka wa Polisi Renatus Zakeo ameiambia mahakama kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 27 mwaka huu.

Alikuwa akiwasomea mashtaka hayo leo Agosti 2 mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Ismail Ngaile.

Mwanafunzi Daniel yeye alikamatwa leo Agosti 2 akiwa shule, akasomewa mashtaka akiwa amevaa sare zake za shule na mkononi akiwa meshika madaftari yake.


Amesema waliiba pikipiki aina ya Toyo mali ya Benjamin Kiboge yenye thamani ya Sh2 milioni.

Washtakiwa wote wamekana mashitaka na wamepelekwa mahabusu hadi Agosti 10 mwaka huu itakapotajwa tena.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.