MADUKA YAFUNGWA,DORIA YATAWALA MITAANI

Wanajeshi wanapiga doria katika barabara za HarareHaki miliki ya picha
Wanajeshi waliojihami wamepiga doria wakiwataka raia kuwa na nidhamu.Watu watatu waliuawa mjini humo siku ya Jumatano wakati wa ghasia kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nelson Chamisa.

Bwana Chamisa alisema siku ya Jumatatu kwamba uchaguzi huo wa Jumamosi ulifanyiwa udanganyifu ili kumpatia rais Mnangagwa ushindi.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.Biashara zimefungwa katika mji mkuu wa Zimbabwe harare huku taifa hilo likisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa.
Matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya upinzani nchini Zibabwe baada ya uchaguzi wa Jumatatu yameichochea jamii ya kimataifa kutoa wito wa kumaliza vurugu.
Umoja wa mataifa na umoja wa ulaya kwa pamoja wamekemea juu vurugu zilizotokea na polisi kufyatua risasi kwa waandamanaji.
Serikali imelaumu upinzani kwa ghasia hizoHaki miliki ya pichaREUTERS
Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri lakini habari zilipozuka kwamba Zanu PF imeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari , hali ilibadilika.
Lakini upinzani wanasema kuwa ZANU PF imeingilia uchaguzi.
Uchaguzi wa Jumatatu ulivutia asilimia 70 ya wapiga kura. Chombo cha habari cha ZBC kimesema kuwa Zec itatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais mwendo wa 12.30 za Zimbabwe.
Baadhi ya raia wa Zimbabwe wakiwa kwenye mstari wa kupiga kura, 70 %ya raia walipiga kura
Image captionTume ya uchaguzi nchini Zimbabwe inasema asilimia 70 ya wazimbabwe walijiandikisha kupiga kura
.Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema kuwa serikali ya Zimbabwe inatakiwa kuhkikisha kuwa vurugu hizo hazitokei.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International linaitaka serikali kufungua mashataka kwa polisi waliofyatua risasi kwa waandamanaji.
''vikosi vya usalama vinapoingilia uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi ya kujieleza'' amesema katibu wa Amnesty.
Nmatokeo gani ambayo yametangazwa hadi sasa?
Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe(Zec) hadi sasa imetangaza ushindi wa viti 140 kwa chama tawala cha Zanu-PF, huku kile cha Muungano wa Upinzani MDC kikiwa na viti 58 , Kulingana na taarifa ya Shirika la Utangazaji la taifa ZBC . Kuna viti 210 Katika Bunge la Taifa la taifa.
Zaidi ya watu milioni tano walijiandikisha kupiga kura, na watu wengi walijitokeza kushiriki uchaguzi kwa kiwango cha 70%.
Ramani ya matokeo kulingana na vyama
Image captio
  • Muungano wa Ulaya umekosoa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya urais .
  • Umesema kuwa ilibaini baadhi ya matatizo, ukiwemo upendeleo wa vyombo vya habari, vitisho kwa wapiga kura na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi , ukiongeza kuwa ''mazingira ya uchaguzi hayakuboreshwa na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa uaminifu ".
  • Hii ni mara ya baada ya miaka 16 kwa serikali kuwaruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya na Marekani kuchunguza uchaguzi
  • Kwa upande wa Muungano wa Afrika, mapema wiki hii umesema kuwa uchagauzi huo ulikuwa huru na wa haki , akiongezea kuwa unaadhimisha wakati muhimu wa mabadiliko ya kisiasa.
  • Ripoti ya awali kutoka waangalizi wa SADC inasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa amani na ulifanyika kulingana na sheria.
  • Wawakilishi wake, waziri wa maswala ya kigeni nchini Angola Manuel Domingos Augusto ameutaja uchaguzi huo kuwa kidemokrasia.
  • Muungano wa Comesa ulisifu tume ya uchaguzi kwa kutumia kifaa cha Biometric kusajili wapiga kura akisema kuwa kimepunguza uwezekano wa watu kupiga kura zaidi ya mara moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527